Matembezi katika mazingara ni njia mojawapo ya kujiburudisha na kupumzika lakini huja na hatari zake vile vile. Mwitu, kama ilivyo bahari, ni mahali nzuri, ya kuvutia na maridadi. Hata Hivyo, uzuri huo huja na tahadharikwa kuwa maeneo haya yaweza kuwa hatari. Twashukuru kwamba mazingara huwa yana njia ya kutuonya dhidi ya majanga haya kabla hayajatendeka. Lakini kam hujui hizi dalili, unaweza kuathirika kutokana na majanga haya hatari sana.
1. Miti Iliyo na Maumbo la-J
Unapopita msituni, labda katika harakati ya kukwea mlima, na ukaona kundi la miti iliyo na umbo la- J, hiyo ni ishara wazi ya kuja kwa maporomoko ya ardhi. Miti hiyo imeinama na kupoteza maumbo yao kwa sababu ya kuporomoka pole pole kwa ardhi. Alahamdhulilahi umekwepa janga.
2. Kupunguka katika kiwango cha maji baharini
Endapo maji katika ufuo wa bara Pacific yameanza kupunguka, unaweza kuwa katika hali hatari ya Tsunami ijayo. Unapaswa kwenda katika maeneo salama haraka. Tsunami kawaida hutokea wakati tetemeko la ardhi hufanyika chini ya maji na maji yaliyo juu kuhamishwa na mawimbi husonga maili 500 kwa kila saa baharini.